Monday, November 7, 2022

UTAJIRI WENYE UCHUNGU- 2

Sehemu Ya Pili (2)


“Ila...au subiri...naomba nikwambie siku nyingine, ila jua kwamba ni kitu kinachoniumiza sana moyoni mwangu...” alisema Dylan, hakutaka kusikia Catherine angesema nini, alichokifanya ni kukata simu, kilichofuatia ni sauti ndogo ya kilio cha kwikwi.

****

Mapenzi yalimuumiza mno, kila siku alikuwa mtu wa kumfikiria Dylan tu, alimpenda mvulana huyo na alikuwa tayari kwa kila kitu. Kitendo cha kumwambia kwamba kulikuwa na kitu alitaka kumwambia lakini akanyamaza, kilimpa mawazo mengi Catherine kiasi kwamba alibaki akiwa na mawazo tele.

Hakutaka kukubali, alichokifanya ni kuchukua simu yake na kuanza kumpigia tena, simu iliita, iliita na kuita lakini haikupokelewa kabisa. Hakutaka kukubali, hakutaka kuona anashindwa, aliendelea kumpigia lakini ikatokea kipindi ambacho simu hiyo haikuwa ikipatikana kabisa.

Kichwa chake kilichanganyikiwa mno, hakutaka kubaki chuoni, kitendo cha mvulana huyo kutokupokea simu kilimchanganya sana, alichokitaka kusikia ni kile ambacho Dylan alitaka kumwambia.

Chuoni hakukukalika tena, alichokifanya ni kuondoka na kuelekea katika stesheni ya treni za umeme na kupanda moja ambayo alitaka impeleke kutoka katika Jiji la Cambridge mpaka Boston alipokuwa akisoma Dylan.

Ndani ya treni alikuwa na mawazo mengi, hakuonekana kuwa na raha kabisa, mapenzi yalikichanganya kichwa chake. Hakukuwa na kitu kingine alichokifikiria zaidi ya Dylan tu.

Baada ya dakika thelathini, treni ikaanza kuingia katika Jiji la Boston, kwa haraka sana Catherine akasimama na kwenda mlangoni, alikuwa na presha kubwa ya kutaka kuteremka, amuwahi rafiki yake wa kiume na kuzungumza naye.

Treni iliposimama, hakutaka kubaki ndani ya treni ile, akatoka na kuanza kuondoka. Alitoka ndani ya jengo la kituo hicho na kufuata teksi moja na kuingia ndani, dereva aliyekuwa nje akisubiri abiria, akaingia ndani.

“Where to?” (Unakwenda wapi?) aliuliza dereva mara baada ya salamu.

“Boston University..”

Dereva akawasha gari na kisha kuanza safari ya kuelekea huko. Njiani, hakutaka kuzungumza kitu chochote, bado aliendelea na jitihada zake za kumtafuta Dylan kwenye simu pasipo mafanikio yoyote yale.

Walichukua dakika ishirini ndipo wakafika katika geti la chuo hicho na kusimamisha teksi, harakaharaka Catherine akalipa na kuteremka. Idadi kubwa ya wanachuo ilikuwa katika eneo la chuo hicho, kila mmoja alionekana kuwa bize huku wengi wakiwa wamekaa kimakundi-makundi wakijadiliana.

Hakutaka kujali sana, alichokifanya ni kuelekea ndani kabisa ambapo huko akaanza kumuulizia Dylan. Jina la mvulana huyo lilikuwa kubwa, uwezo wake darasani ulimfanya watu wengi kumfahamu, wengi walimuita kwa jina la kompyuta kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao.

“Mmh! Sijui kama yupo...”

“Kwani leo hajaonekana?”

“Nilimuona kwenye uwanja wa kikapu, baada ya hapo, kuna watu walimfuata, sijui ameelekea wapi,” alisema mwanaume aliyeulizwa na Catherine.

“Wanaume gani?”

“Siwafahamu, walikuwa na miili mikubwa, sidhani kama kuna usalama...”

“Sawa! Nashukuru!”

Japokuwa alimkosa Dylan chuoni lakini hakutaka kuondoka Boston, lengo lake kubwa lililomtoa Cambridge na kumpeleka Boston lilikuwa ni kuonana na mvulana huyo tu. Alihisi kulikuwa na tatizo, hakuwa tayari kuondoka na kurudi chuo, iwe isiwe ilikuwa ni lazima kumuona.

Ilipofika saa mbili usiku, akasikia simu yake ikiita, kwanza akahisi kwamba walikuwa wazazi wake ambao walikuwa na kawaida ya kumpigia simu kila siku usiku, alipoichukua simu na kuangalia kioo, hakuamini, alikuwa Dylan.

“Halo Dylan...” aliita Catherine.

“Upo wapi? Chuo au nyumbani?” ilisikika sauti ya Dylan.

“Nipo hotelini...”

“Hotelini?”

“Ndiyo!”

“Unafanya nini?”

“Nimekuja kukuona!”

“Kwa hiyo upo Boston?”

“Ndiyo!”

“Hoteli gani?”

“San Marino...”

“Sawa! Ngoja nije nikuone...”

“Kweli?”

“Ndiyo! Nipe dakika kadhaa, nina habari njema...”

“Ipi hiyo?”

“Usijali rafiki, nakuja...”

Catherine alijikuta akishusha pumzi ndefu na kuachia tabasamu pana, hakuamini kile alichokisikia kwamba mvulana aliyekuwa akimpenda alikuwa njiani kuelekea katika hoteli ile aliyokuwepo.

Tangu mara ya mwisho kuonana naye katika ikulu ya Marekani, hakuwahi kuonana naye tena mpaka kipindi hicho. Miaka miwili ilikuwa imepita, hakuwahi kumuona zaidi ya kuwasiliana naye kwenye simu tu.

Baada ya dakika arobaini na tano, simu ya mezani ikaanza kulia, akaifuata, akaipokea, sauti aliyoisikia ni ya dada wa mapokezi ambaye alimpa taarifa kwamba kulikuwa na mgeni wake aliyetaka kumuona.

“Mwambie aje...”

Catherine akajiweka vizuri chumbani kwake, akavaa nguo ya kulalia harakaharaka kwani siku hiyo, tena katika usiku kama huo ndiyo ilikuwa yenyewe ya kumfanya Dylan awe mpenzi wake kwa namna alivyojipanga kumtega hasa kwa mikao ya ajabu-ajabu kitandani.

Baada ya dakika kadhaa, akasikia mlango ukigongwa, kwa kuwa alikuwa ameshauacha wazi, akamkaribisha mgongaji, Dylan akaufungua mlango na kuingia ndani. Hali aliyomkuta msichana huyo haikuwa ya kawaida, alivalia nguo ya kulalia iliyoonyesha maungo yake ya ndani, mpaka nguo ya ndani, nyekundu aliyoivaa, ilionekana vizuri.

“Karibu Dylan,” alisema Catherine kwa sauti nyembamba ambayo aliamini ingezisismua ngoma za masikio ya Dylan.

Dylan akameza mate, akabaki akimwangalia Catherine kwa macho yenye matamanio lakini usiku huo alitaka kupinga kufanya naye kitu chochote kile, hakuwa mpenzi wake japokuwa alijisikia hali ya tofauti sana moyoni mwake.

“Kuna nini mpe...Dylan?” aliuliza Catherine.

“Sikiliza, nimechaguliwa kujiunga na timu ya mpira wa kikapu ya Boston...” alisema Dylan huku akitoa tabasamu pana.

“Unasemaje?”

“Ninakwenda kuwa bilionea Catherine, ninakwenda kutajirika...” alisema Dylan kwa sauti kubwa, Catherine aliyekuwa kitandani akasimama na kumsogelea, kilichofuatia ni kumkumbatia kwa nguvu kana kwamba hakutaka atoke mikononi mwake.

“Dylan....” aliita Catherine.

“Nipo hapa...”

“Ninakupenda sana...” alisema Catherine.

“Unasemaje?”

“Ninakupenda...”

“Mimi?”

“Ndiyo!”

“Masikini mimi?”

“Ndiyo! Ninakupenda sana, naomba uwe wangu...”

“Niwe wako mimi?”

“Ndiyo!”

“Hapana Catherine...”

“Kwa nini?”

“Sikiliza Catherine, nina maana yangu kukwambia hivyo...” alisema Dylan.

Dylan akajitoa katika mikono ya Catherine, japokuwa msichana huyo alitamani waendelee kukumbatiana lakini kwa Dylan hakutaka kabisa kuendelea kuwa hivyo kwani isingeleta picha nzuri na wakati hakutaka kabisa kuwa mpenzi wake.

“Naomba uniache Catherine, siwezi kuwa mpenzi wako...” alisema Dylan huku akimtoa msichana huyo mikononii mwake, maumivu aliyoyasikia Catherine moyoni mwake, hayakuweza kusimulika.


Catherine hakutaka kuamini alichokisikia, moyo wake ulikuwa kwenye mapenzi ya dhati kwa mwanaume huyo ambaye alimpenda kwa moyo wake wote. Kila alipomwangalia, alizidi kumpenda ila maneno aliyomwambia kwamba hawezi kuwa naye, yalimchanganya.

Alishindwa kuvumilia kabisa, hapohapo machozi yakaanza kumtoka machozi mwake na kutiririka mashavuni mwake. Alisafiri kutoka Cambridge mpaka Boston kwa ajili ya kumwambia mwanaume huyo kwamba alikuwa akimpenda, alipoufikisha ujumbe wake huo, eti mwanaume huyo akamwambia kwamba hawezi kuwa mpenzi wake.

“Dylan, ninakupenda sana, naomba uwe wangu,” alisema msichana huyo huku akionekana kuumia moyoni mwake.

“Catherine, haujui ni kitu gani kinaendelea katika maisha yangu,” alisema Dylan kwa sauti ya chini, alionekana kuwa na huzuni mno.

“Kitu gani?”

“Ndiyo maana nakwambia achana na mimi, mbali na umasikini, sitokufanya uyafurahie mapenzi...” alisema Dylan.

“Dylan, nakuomba tafadhali, naomba uwe wangu,” alisema msichana huyo.

Japokuwa Catherine aliomboleza kwa kumtaka mwanaume huyo awe naye lakini hilo halikuwezekana hata kidogo, bado aliendelea kusisitiza kwamba hakutaka awe mpenzi wake hivyo aachwe kama alivyokuwa.

“Naomba nikuulize swali...” alisema Catherine.

“Uliza...”

“Unanipenda?”

“Ndiyo! Ninakupenda sana Catherine...”

“Namaanisha kimapenzi...unanipenda?”

“Na mimi nimemaanisha kimapenzi, ninakupenda mno,” alisema Dylan.

“Kwa nini hutaki kuwa mpenzi wangu?” aliuliza Catherine.

“Kwa sababu sitaki ulie, hilo tu...”

“Hutaki nilie, kwa sababu gani? Una msichana mwingine?”

“Sina na sitegemei kuwa na msichana yeyote katika maisha yangu, nitabaki peke yangu milele, ila suala la kuwa nawe, haliwezekani,” alisema Dylan huku macho yake tu yakionyesha ni jinsi gani alimaanisha alichokisema.

Hakupata alichokitaka, alikuwa mnyonge na wala hakutaka kukaa huko Boston, alichokifanya ni kuondoka zake na kurudi New York kwani kwa jinsi alivyochanganyikiwa, asingeweza kabisa kurudi chuoni na kusoma.

Njiani, ndani ya ndege, alikuwa na mawazo lukuki, hakukuwa na siku ambayo moyo wake uliumia kama siku hiyo, hapo kabla alikuwa na uhakika kwamba angeanzisha uhusiano wa kimapenzi na Dylan lakini kitu alichokutana nacho huko kilimnyong’onyeza na hakuwa na nguvu hata kidogo.

*****

“Amefanana na mimi?” aliuliza Bwana James.

“Ndiyo! Amefanana na wewe, kama mapacha,” alisema bi Claire huku akimwangalia mume wake usoni.

“Anaitwa nani?”

“Dylan Christopher, ni mrefu kama wewe...”

“Hahaha! Basi tutakuwa wawili-wawili...” alisema Bwana James.

Bi Claire aliamua kumtaarifu mume wake juu ya mfanano aliokuwa nao na kijana ambaye walikutana naye wakati walipokwenda Ikulu kula chakula na rais. Bwana James alipoambiwa, alionekana kuwa mwenye furaha tele hasa baada ya kuona kwamba hata watu aliokuwa nao, wote walimfananisha na huyo kijana.

Mawazo juu ya kijana huyo yalimsumbua kichwani mwake, alitamani kuonana naye hata siku moja lakini kutokana na ubize mkubwa aliokuwa nao, alishindwa kabisa. Kila siku alikuwa mtu wa kukaa ofisini mwake, mezani kulikuwa na mafaili mengi yaliyokuwa na karatasi ambazo alitakiwa kuziandika na kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kinavyotakiwa kwenda.

Fedha hazikuisha, kila siku ziliendelea kuingia katika akaunti yake na kumfanya kuwa bilionea mkubwa. Aliyakumbuka maisha aliyoishi kabla, yalikuwa ya kimasikini ambapo alishindwa hata kupata dola mia tano.

Hakutaka kuishi maisha hayo tena, alitaka kupata fedha zaidi na kumfanya kuwa tajiri mkubwa baadaye. Alihakikisha familia yake ikipata kila kitu, hakutaka kuiona ikiteseka au ikipata matatizo yoyote yale.

Maisha yaliendelea, mwaka wa kwanza ukapita, wa pili ukaingia na ndipo mawazo juu ya huyo kijana yalipoanza kurudi tena kichwani mwake. Hakujua ni kwa sababu gani lakini kila siku alipokuwa akikaa ofisini mwake, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumfikiria kijana huyo, mawazo juu yake yaliendelea kumtesa kila siku.

“Huyo kijana yupo wapi?” aliuliza Bwana James.

“Catherine alisema yupo Boston...”

“Ninataka kuonana naye, mawazo juu yake yamekuwa yakinitesa sana, au hata picha zake unazo?” aliuliza Bwana James.

“Hapana, ila nina uhakika Catherine anazo...”

“Hebu mpigie simu...”

Bi Claire akafanya kama alivyoambiwa, akampigia simu binti yake lakini haikuweza kupatikana zaidi ya kuambiwa aache ujumbe mfupi wa maneno. Hakuacha ujumbe wowote ule, akaikata simu kwa lengo la kujaribu hapo baadaye.

Baada ya kupita saa mbili, binti yao, Catherine akarudi nyumbani hapo. Kwanza kila mmoja alishangaa, muda huo alitakiwa kuwa chuoni, wakati wanajiuliza hilo, wakagundua kwamba binti yao hakuwa sawa kabisa, alionekana kuwa na mawazo tele, tena hata macho yake yaliwatisha, yalikuwa mekundu hali iliyoonyesha kwamba muda mchache uliopita alikuwa akilia.

“Kuna nini?” aliuliza mama yake. Catherine hakujibu zaidi ya kuelekea chumbani kwake.

Wakahisi kulikuwa na tatizo, alichokifanya bi Claire ni kumfuata binti yake, alitaka kufahamu ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea mpaka kumrudisha nyumbani tena huku akionekana kuwa na huzuni.

“Moyo unaniuma mama...” alisema Catherine huku akiyafuta machozi yake.

“Kuna nini?”

Mama yake alikuwa kila kitu katika maisha yake, alimchukulia kama rafiki yake wa karibu na kila kitu kilichomsumbua, hakumficha, alimwambia ukweli.

Alichokifanya Catherine ni kumwambia mama yake kila kitu kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake, alimwambia ukweli kwamba alimpenda sana Dylan tangu siku ya kwanza alipokutana naye, akajitahidi kuwa naye karibu na hatimaye kutamani kuwa mpenzi wake.

“Sasa kipi kinakuliza?” aliuliza mama yake.

“Amenikataa, amesema hataki kuwa mpenzi wangu,” alijibu Catherine huku akilia kama mtoto.

Mama yake akawa na jukumu kubwa la kumbembeleza binti yake. Alimuonea huruma, alikuwa binti yake wa kwanza hivyo kumuona akilia huku akiteseka moyoni mwake, hakika ilimuuma mno.

“Nyamaza, baba yako atakusaidia...” alisema bi Claire kwa sauti ya chini.

“Baba atanisaidia?”

“Ndiyo! Anataka kwenda kuonana naye, nitamwambia kuhusu hilo pia, atakusaidia,” alisema bi Claire huku akimfariji binti yake.

Alichokifanya mwanamke huyo ni kuelekea sebuleni ambapo akamkuta mume wake akiwa ametulia kochini huku akionekana kuwa na mawazo lukuki. Kwa mwendo wa taratibu akamsogelea na kuanza kuzungumza naye.

“Kuna nini?” aliuliza Bwana James.

“Catherine analia...”

“Kisa?”

Bi Claire hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kuanza kumuhadithia mume wake kile alichoambiwa na binti yake kule chumbani. Bwana James alihuzunika, katika maisha yake hakutaka kabisa kuona binti yake akilia, hivyo kitendo cha kusikia kwamba binti yake alilia kisa tu kukataliwa na huyo Dylan, ilimuuma mno.

“Tuna fedha, unalijua hilo?” aliamua kumuuliza mke wake.

“Ndiyo!”

“Kama tuna fedha, kipi kinashindikana? Kununua mapenzi?” aliuliza mzee huyo.

“Hakuna kinachoshindikana!”

“Basi ni lazima tukutane na huyo Dylan haraka iwezekanavyo, sipendi kumuona binti yangu akiwa na huzuni, sipendi kumuona akilia,” alisema Bwana James.

Huo ndiyo ulikuwa ukweli, alimpenda mno binti yake mkubwa hata zaidi ya alivyompenda binti yake mdogo, Laura. Kwake, msichana huyo alikuwa kila kitu kitendo cha kuambiwa kwamba alikuwa akilia kisa tu kulikuwa na mwanaume alimkataa, ilimchanganya akili yake.

Aliamini katika fedha kwamba unapokuwa na fedha hakuna kitu chochote kile kinachoshindikana hivyo kama huyo Dylan amekataa kuwa na binti yake, aliamini kama angetumia fedha basi ingekuwa rahisi kwake kumpata na kumuingiza katika mikono ya binti yake.

“Mwambie tunamfuata, tutazungumza naye,” alisema Bwana James huku akionekana kumaanisha alichokisema.

Catherine alipopewa taarifa juu ya kile alichoambiwa, kidogo moyo wake ulikuwa na ahueni kwani hata yeye aliamini kwamba fedha zingeweza kubadilisha kitu chochote kile.

Wakapanga siku ya safari, haikuwa wiki hiyo ila ingefanyika wiki mbiliz zinazofuata. Katika kipindi chote cha kusubiria hiyo safari, bado Catherine alikuwa akiwasiliana na Dylan huku akimsisitiza awe mpenzi wake lakini mwanaume huyo alikataa kwa kusema kwamba alikuwa na sababu yake kubwa, ila ya pili, hakutaka kumuona msichana huyo akiwa kwenye majonzi makubwa.

Siku zikaendelea kukatika, baada ya wiki moja, hapo ndipo familia hiyo ikapanda ndege binafsi na kuelekea Boston. Njiani, walikuwa wakizungumza lakini kichwa cha Catherine kilikuwa na mawazo tele, hakuamini kama kweli Dylan angeweza kukubaliana naye na hatimaye kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Wazazi wake waliendelea kumfariji kwa kumwambia kwamba kila kitu kingewezekana kwani fedha ndicho kitu kilichokuwa na mafanikio makubwa kama tu kingetumika kama kinavyotakiwa.

Walichukua saa mbili, ndege ikatua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Boston ambapo wakateremka na kuanza kwenda hotelini huku wakiwa wamepokelewa kwa magari maalumu, ya kifahari ambayo hayakuwa na uwezo wa kupenyeza risasi.

Bwana James alikuwa bilionea mkubwa, kila alipopita, alinukia fedha, alikuwa mtu anayelindwa sana nchini Marekani kiasi kwamba hata wabaya wake kumpata ilikuwa kazi kubwa.

Baada ya kufika katika hoteli ambayo waliweka oda kwa kuchukua hoteli nzima, wakatulia vyumbani mwao. Japokuwa kwa upande wa Bwana James alionekana kama kupoteza muda, ila alifanya hivyo kama njia mojawapo ya kumfanya binti yake awe na furaha maishani mwake, hakutaka kumuona akilia au akiteseka maishani mwake, kwa kifupi, hakutaka kumuona binti yake huyo akilia kwa uchungu.


Maisha hayakuwa mazuri hata mara moja, kila siku bi Leticia alikuwa mtu fukara ambaye hakuwa na kiasi chochote cha fedha, hakuwa akifanya biashara yoyote, hakuwa na kazi ila kitu pekee alichokuwa akikifanya katika maisha yake ni kuamka asubuhi, siku ya Jumapili, anawahi kanisani na kusafisha kanisa.

Hiyo ndiyo ilikuwa kazi pekee aliyokuwa akiifanya. Mume wake alipofariki, kila kitu kikaenda vibaya, hakuwa na fedha za kutosha, fedha ambazo alikuwa akizitegemea ni zile walizokuwa wakilipwa wajane ambazo zilikuwa katika mpango wa serikali ya Marekani.

Hata alipompata Dylan, hakukuwa na kitu kilichobadilika, maisha ya ufukara yaliendelea na fedha alizokuwa akipewa na serikali ndizo zilizokuwa zikitumika katika mambo mengine.

Mtoto Dylan akakua na kukua, akaanza masomo yake katika shule ya kimasikini hapo Kenner ambapo huko walimu wakagundua kitu kwamba mbali na umasikini uliokuwa ukimtafuna yeye na bi Leticia ambaye kila siku alijua huyo ndiye mama yake, lakini kichwa chake kilikuwa tofauti na watoto wengine.

Alikuwa na akili mno, alikuwa mwanafunzi wa kwanza kujua kusoma na kuandika, hakuwa muongeaji sana wala msomaji sana lakini kila alipoingia darasani, walimu waliushangaa uwezo wake.

Mpaka anafikisha umri wa miaka kumi na nne, muda wa wavulana wengi kubalehe, kwa Dylan hakuwahi kuona mabadiliko yoyote yale, alikumbuka vilivyo kwamba mwalimu wake alimwambia mara atakapofikia umri huo ndipo hapo angeweza kuona akiingia katika balehe lakini mpaka kipindi hicho, kukawa kimya.

Alishangaa, alishtuka, alihuzunika mno lakini hayo yote hayakuweza kubadilisha kitu chochote kile. Hakutaka kukaa kimya, alichokifanya ni kumwambia bi Leticia kile kilichokuwa kikiendelea ambapo mwanamke huyo alishangaa sana, akamchukua na kumpeleka hospitali.

“First of all, he has impotence problem,” (Kwanza kabla ya yote, ana tatizo la kutokusimamisha uume) alisema daktari maneno yaliyomshtua bi Leticia.

“What did you just say?” (Umesemaje?)

“He has impotence problem,” (Ana tatizo la kutokusimamisha uume wake) alijibu tena daktari.

Bi Leticia akaonekana kushtuka, hakuamini kile alichokisikia, alichokifanya ni kuchukua karatasi iliyoandikwa ripoti ile ili ajionee kama kile alichoambiwa ndicho kilichoandikwa au la.

Majibu aliyopewa na kile kilichoandikwa kwenye ripoti hakikuwa na tofauti yoyote yale, ukweli ukawa kwamba Dylan alikuwa na tatizo la kutokusimamisha uume wake. Bi Leticia alihisi kuchanganyikiwa, moyo wake ukamuuma mno, duniani, yeye akajiona kuwa miongoni mwa watu wenye mikosi, alikuwa masikini, mjane na mwisho wa siku Mungu kumpa mtoto katika njia ya ajabu sana, ila pamoja na baraka hiyo, mtoto huyo alikuwa kwenye matatizo kiafya.

Daktari hakuishia hapo, alichokifanya ni kumuita bi Leticia ndani ya ofisi yake kisha kuanza kumpa elimu kamili kuhusu ugonjwa huo. Bi Leticia alibaki akimsikiliza lakini akili yake haikuwa hapo kabisa, alikuwa akimfikiria Dylan tu, jinsi atakavyoishi huko baadaye.

“Hili ni tatizo ambalo huwatokea watu wengi. Tatizo hili hutokea mara baada ya mtu kuumwa magonjwa hatari kama kisukari, kupooza ila na wengine huzaliwa nalo kama ilivyokuwa kwa Daylan...” alisema daktari yule na kumeza mate kisha akaendelea:

“Kuwa na tatizo hili haimaanishi kwamba utakufa, hauwezi kufa bali utaishi. Hii inamaanisha kwamba huyu Dylan hatokufa bali ataendelea kuishi,” alisema daktari maneno ambayo aliamini yangemtia moyo mwanamke huyo.

Bi Leticia alichanganyikiwa, hakutaka tena kubaki mahali hapo bali alichokifanya ni kumchukua Dylan na kuondoka naye. Majibu yale alipewa yeye kama yeye, kijana huyo hakujua ni kitu gani kilitokea lakini kitendo cha kumuona mama yake akiwa kwenye hali hiyo, akashangaa mno.

Alijaribu kumuuliza, alitaka kujua ni kitu gani kilindelea lakini bi Leticia hakutaka kujibu, alibaki kimya. Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza, kila alipomwangalia Dylan moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hakutaka kuona jambo hilo likiendelea mwilini mwa Dylan lakini hakuwa na jinsi, wakati mwingine aliona kuwa na umuhimu wa kukubaliana na kila kitu.

Hata kabla Dylan hakufikisha miaka kumi na nane, akagundua kwamba alikuwa na tatizo hilo, hakuwa kama marafiki zake, jambo hilo lilimuuma mno, lilimliza kila siku, moyo wake uliumia kupita kawaida ila pamoja na kutokwa na machozi, moyo kuumia lakini hakukuwa na kilichobadilika.

Baada ya kugundua kwamba alikuwa na tatizo hilo, Dylan hakujishughulisha na wanawake, muda mwingi alikuwa akikaa na marafiki zake, wakizungumza, alicheka kwa furaha lakini kila alipokuwa peke yake, moyo wake ulikuwa kwenye uchungu mkubwa.

Hali hiyo iliendelea mpaka alipokutana na msichana Catherine. Ni kweli alimpenda msichana huyo ila kitu kilichosababisha kuwa naye ni hilo tatizo alilokuwa nalo. Lilimnyima raha, alikosa amani na hakukuwa na kitu alichokitamani kwa kipindi hicho kama kuwa na msichana huyo.

“Kwa hiyo hilo ndilo tatizo linalokukabili?” aliuliza Bwana James.

“Ndiyo! Najiona kuwa si kitu, ni mwanaume jina ila sijakamilika,” alisema Dylan huku akionekana kuwa na majonzi.

“Hapana! Nahisi hili tatizo linaweza kutibika, ni lazima nifanye kila liwezekanalo mpaka kuhakikisha unapona,” alisema Bwana James.

“Kweli?”

“Ndiyo!”

“Unaamini nitapona?”

“Asilimia mia moja, nina madaktari waliobobea nchini China ambao wanafanya tiba kwa dawa za mitishamba, huko utafanikiwa tu, ni lazima twende,” alisema Bwana James.

Alivyoambiwa hivyo, kidogo Dylan akaonekana kuwa na tumaini, mzee huyo akaonekana kuwa msaada wake mkubwa. Hakutaka kuchelewa, kwa kuwa alikuwa na uhitaji mkubwa, akaomba ruhusa katika klabu yake na kisha kuanza safari ya kuelekea huko huku akiongozana na Bwana James, tena kwenye ndege yake binafsi ya kitajiri.

“Ila naomba nikuulize swali...”

“Uliza tu!”

“Una uhakika utamuoa binti yangu ukitibiwa kwa gharama zangu?” aliuliza mzee huyo.

“Ndiyo! Nitamuoa, nakuhakikisha hilo,” alisema Dylan.

“Ni lazima tuweke mkataba, haiwezekani nikafanikisha utibiwe halafu mwisho wa siku unigeuke, ninampenda sana binti yangu na ndiyo maana najitolea kukusaidia kwa ajili yake,” alisema mzee huyo.

Alikuwa mfanyabiashara anayejua sana kuhusu mikataba, hakutaka kukubaliana na mtu mdomo kwa mdomo bali ilikuwa ni lazima makubaliano yaandikwe kwamba mara baada ya kumtibia basi amuoe binti yake, kweli mkataba ukaandikwa.

Walichukua zaidi ya saa ishirini na moja ndipo wakaingia jijini Beijing ambapo wakashuka na kuanza kuelekea hotelini. Alichokifanya Bwana James ni kuwasiliana na daktari wake wa tiba za asili ambapo akamwambia kwamba alikuwa nchini humo na mgonjwa wake hivyo alihitaji matibabu hayo.

“Hakuna tatizo...mlete...”

Dylan alikuwa mwenye furaha tele, moyoni mwake hakuamini kama kweli huo ndiyo ulikuwa mwisho wa matatizo yake. Aliamini dawa za mitishamba za Kichina, alijua namna zilivyokuwa zikifanya kazi kwa uwezo mkubwa sana, hivyo tumaini lake lote lilikuwa katika dawa hizo.

Baada ya kukaa hotelini kwa usiku mmoja, kesho yake wakaondoka na kuelekea katika kijiji cha Nanjing ambacho kilikuwa Kaskazini mwa nchi hiyo. Kutoka hapo Beijing, walichukua saa nne njiani na ndipo wakafika katika kijiji hicho ambapo wakapokelewa na kwenda kwa mzee maarufu wa kutibu watu kwa kutumia mitishamba.

“Karibuni sana...” alisema mzee huyo ambapo kila neno alilolizungumza, kulikuwa na mkalimani kutoka lugha ya Kichina kwenda Kingereza.

Mpaka kufikia hapo, Dylan alikuwa na uhakika wa kupona tatizo lake na hatimaye kumuoa msichana Catherine.


Nyumbani hawakutulia, kila wakati Catherine alikuwa akipiga simu kwa baba yake kujua walifikia wapi, kama Dylan alikubali au alikataa. Moyo wake haukuwa na amani hata kidogo, hakutulia, alijifikiria kuhusu mvulana huyo, alimpenda mpaka hatua ya mwisho kabisa ambapo akipenda zaidi ya hapo angechanganyikiwa na kuwa kichaa.

Saa zikaendelea kukatika, kila alipomuuliza baba yake waliishia wapi, alimwambia asubiri kwani bado kulikuwa na vitu vichache vya kufanya. Catherine akatulia, akajipa moyo kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima baba yake akamilishe kile kitu, hivyo akatulia.

Siku hiyo ilipokatika, Bwana James akawapigia simu na kuwaambia kwamba ni lazima waondoke waelekee nchini China kwani kulikuwa na kitu hakikukaa sawa. Hilo liliwachanganya Catherine na mama yake, hawakuelewa ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea kwani hata safari hiyo ilikuwa ya ghafla sana.

“Kuna nini?” aliuliza bi Claire.

“Kuna kitu mke wangu!”

“Ni salama lakini?”

“Ndiyo! Wala msijali...”

“Na huyo kijana amesemaje? Atamuoa?”

“Hilo ndilo tunalizungumzia, ila kama tukifanikisha kukifuata kile tunachokifuata nchini China, atamuoa tu,” alisikika Bwana James.

“Kitu gani hicho?”

“Usiwe na hofu mke wangu! Nitakujulisha tu,” alisema Bwana James na kukata simu.

Kitendo cha kuambiwa na mume wake kwamba kulikuwa na kitu ambacho hakutakiwa kukifahamu, kilimfanya kuwa na wasiwasi mkubwa, akakosa amani kwa kuona kwamba kulikuwa na kitu kibaya ambacho mumewe hakutaka akifahamu. Hilo hakujali, hakumwambia binti yake, akabaki nalo moyoni na siku kuendelea mbele.

Upande wa pili, tayari mzee huyo wa dawa za mitishamba akaanza kufanya mambo yake, alihakikisha anamchunguza kwa umakini kujua tatizo lilikuwa nini kwani hakutakiwa kufanya kazi hiyo pasipo kujua historia fupi ya mgonjwa.

“Mtoto wako alianza lini hili tatizo?” aliuliza mzee huyo kupitia mkalimani, tena mbele ya Dylan mwenyewe.

“Alizaliwa nalo.”

“Na ilikuwaje katika kipindi chake cha utotoni? Nataka nipate historia kidogo kutoka kwako mzazi,” alisema mzee yule.

“Huyu si mtoto wangu, ni rafiki yangu!”

“Siyo mtoto wako?”

“Ndiyo!”

“Mmh! Mbona mmefanana hivyo?”

“Hutokea tu, ila ni rafiki yangu!”

Si mzee yule aliyeshangaa bali hata mkalimani naye akapigwa na mshangao. Kila alipowaangalia watu hao, walionekana kuwa kama mapacha, walifanana kwa asilimia kubwa sasa kitendo cha kuambiwa kwamba watu hao hawakuwa ndugu, kiliwashangaza wote.

“Basi ni lazima mama yake au baba aje hapa, ninataka kujua historia yake kwanza juu ya afya yake,” alisema mzee huyo.

“Hakuna tatizo! Atafika ndani ya siku mbili!”

Hilo wala halikuwa tatizo, walichokifanya ni kuwasiliana na bi Leticia na kumhitaji nchini China. Bwana James ndiye alisimamia kila kitu, akawasiliana na watu wake nchini Marekani na kuwaambia kile alichokitaka.

Kutafuta hati ya kusafiria wala halikuwa tatizo kwani kila mtu alimfahamu na aliheshimika sana. Baada ya siku mbili, Bi Leticia alikuwa ndani ya ndege akielekea nchini China.

Yeye mwenyewe hakuelewa ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea, aliposikia kwamba anahitajika na mzee huyo bilionea, moyo wake ukawa na wasiwasi mno kwa kuhisi inawezekana kulikuwa na kitu kibaya kilichokuwa kimetokea ambacho kilimtia hatihani kijana wake.

Baada ya zaidi ya saa ishirini, alikuwa akiingia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing ambapo akateremka na kupokelewa na watu ambao waliandaliwa na kumchukua na kumpeleka ndani ya gari moja na safari ya kuelekea kijijini kuanza.

Walichukua saa nne ndipo wakaingia ndani ya kijiji hicho. Wakapokelewa vizuri na kupelekwa ndani ambapo Bi Leticia akakutana na kijana wake, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumkumbatia.

“Umefanya nini Dylan mtoto wangu?” aliuliza Bi Leticia huku akimwangalia Dylan usoni, machozi yalikuwa yakimbubujika.

“Sijafanya kitu mama!”

“Sasa kwa nini upo huku?”

“Huyu mzee anataka kushughulikia tatizo langu,” alijibu Dylan.

Miongoni mwa watu walioshtuka, hata Bi Leticia naye alishtuka, alipomuona Bwana James, jinsi alivyofanana na kijana wake alibaki akishangaa. Kipindi cha nyuma aliwasikia baadhi ya vijana wakisema kwamba kijana wake alifanana sana na bilionea huyo, alibisha lakini siku hiyo ndipo akakutana naye, walifanana kwa kiasi kubwa sana na ilikuwa rahisi kusema kwamba ni mapacha.

Hapohapo mzee wa tiba akawaita, wote watatu wakaingia ndani ya chumba kimoja ambapo huko akamtaka Bi Leticia kusimulia historia fupi kuhusu Dylan na jinsi hali ilivyokuwa ikiendelea katika ukuaji wake.

“Wewe kama mzazi utakuwa unafahamu vingi, tatizo lake uliligundua kipindi gani?” aliuliza mzee huyo.

“Kipindi fulani, alipokuwa na miaka kumi na nne...” alijibu.

“Ulimzaa huyu mtoto akiwa mzima wa afya?”

“Hapana!”

“Unamaanisha alikuwa akiumwa? Alikuwa akiumwa nini?” aliuliza mzee huyo, Dylan na Bwana James walikuwa kimya wakimsikiliza.

“Sikumzaa mimi!” alisema bi Leticia huku akiangalia chini, alijisikia uchungu sana kuzungumza maneno hayo kwani katika maisha yake yote mpaka kipindi hicho, Dylana aliamini kwamba huyo alikuwa mama yake wa kumzaa.

“Hukumzaa wewe?”

“Ndiyo!”

“Kwa hiyo wewe si mama yake?”

“Ndiyo!”

Mapigo ya moyo wa Dylan yalikuwa juu, hakuamini kile alichokisikia kutoka kwa mwanamke huyo kwamba hakuwa mama yake. Katika kipindi chote cha maisha yake alifahamu kwamba huyo alikuwa mama yake, sasa ilikuwaje tena aseme kwamba yeye hakuwa mama yake, na kama yeye si mama yake, mama yake alikuwa nani na kwa nini alimficha kwa kipindi chote hicho.

“Naomba unisamehe Dylan, sikutaka ulijue hili,” alisema bi Leticia huku akianza kububujikwa na machozi.

“Sijaelewa mama...”

“Sikukuzaa....”

“Hukunizaa?”

“Ndiyo! Mimi si mama yako!”

“Wewe si mama yangu?” aliuliza Dylan.

Bi Leticia hakujibu swali hilo, tayari machozi yaliongezeka na kuanza kulia kilio cha kwikwi, hakukuwa na mtu aliyechanganyikiwa kama Dylan, kila alipomwangalia mwanamke huyo na maneno aliyokuwa akiyasema, hakuamini, wakati mwingine aliona kama anadanganywa.

Huo ulikuwa ni wakati wa Dylan kufahamu ukweli juu ya kile kilichokuwa kimetokea, Bi Leticia hakutaka kuficha, akaanza kuwahadithia kuanza siku ya kwanza walipokuwa kanisani, tsunami ilipopiga, ilipoliharibu Jiji la New Orleans kwa kujaa maji mpaka baadaye kumuokota mtoto Dylan akiwa kwenye friji.

Alipofikia hapo tu, Bwana James akapigwa na butwaa, akasimama kutoka alipokuwa, akamwangalia Dylan mara mbilimbili, hakuamini kabisa kile alichokisikia. Kila mtu aliyekuwa mahali hapo alibaki akimwangalia mzee huyo ambaye alionyesha wazi kwamba alichanganyikiwa kwa furaha.

“Dylan ni mtoto wangu!” alisema Bwana James huku akionekana kutokuamini.

Kila mtu akabaki akimwangalia mzee huyo, bado hawakufahamu ni kitu gani kilimtokea mpaka kupagawa kiasi hicho. Bwana James akainama na kumshika Dylan, hapohapo akamkumbatia, akamng’ang’ania kama mtu ambaye hakutaka kutoka mikononi mwake.

Si Bi Leticia aliyeshangaa, kila mtu aliyekuwa ndani ya chumba hicho alishangaa mpaka mkalimani mwenyewe. Bwana James alikuwa akibubujikwa na machozi, hakuamini kama kuna siku angekutana na mtu huyo, mtoto wake ambaye alimuhifadhi ndani ya friji na hatimaye mpenzi wake, Catherine kufariki miaka mingi iliyopita.


Kila mmoja alibaki kimya ndani ya chumba kile na ni Bwana James peke yake ndiye aliyekuwa akizungumza. Kila mmoja alimshangaa, kitendo chake cha kumkumbatia Dylan huku akisema kwamba kijana huyo alikuwa mtoto wake, walimshangaa.

Hawakutaka kuzungumza lolote lile, walihisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea hivyo kusubiri ni kitu gani kingetokea baada ya hapo. Bwaja James aliendelea kumkumbatia kwa fuara mpaka baada ya dakika tano, akamuachia huku machozi yakimbubujika mashavuni mwake.

“What is going on?” (Nini kinaendelea?) aliuliza bi Leticia.

“He is my son,” (Ni kijana wangu) alijibu.

“Your son?” (Kijana wako?)

“Yes!”

Kila mmoja alishangaa, maneno aliyoongea yaliwachanganya, ilikuwaje mtu huyo aseme kwamba huyo alikuwa kijana wake na wakati hawakuwa hata ndugu? Hapo ndipo Bwana James alipoanza kuhadithia kila kitu kilichotokea siku ya nyuma, kipindi kile tsunami ilipotokea mpaka mpenzi wake kufariki dunia na yeye kumuweka mtoto katika friji.

“Sikuwa na jinsi, sikuwa tayari kumuona mtoto wangu akifariki hivyo nilichokifanya ni kuchukua friji na kumuingiza ndani,” alisema Bwana James na kuendelea.

Alisimulia kila kitu mpaka namna alivyonusurika na mwisho wa siku kukutana na msichana Catherine na hivyo kuanza uhusiano wa kimapenzi na mwisho wa siku kumuoa na kupata mtoto aliyempa jina la Catherine ambalo lilikuwa ni kama kumuenzi mpenzi wake wa zamani.

“Wewe ni baba yangu?” aliuliza Dylan huku akionekana kutokuamini.

“Ndiyo! Wewe ni mtoto wangu wa kwanza...nilijua nimekupoteza na nisingekuona tena,” alisema Bwana James.

Moyo wake ulijawa na furaha tele, hakuamini kwamba mara baada ya miaka mingi kupita tena huku akiwa amemtelekeza mtoto wake katika friji hatimaye siku hiyo angeonana naye.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo, Dylan alifanyiwa matibabu na kisha kuruhusiwa kuondoka huku akitakiwa kunywa dawa alizopewa kwa ajili ya afya yake. Hilo halikuwa tatizo, hivyo wakaanza safari ya kurudi nchini Marekani.

Muda wote Bi Leticia alikuwa kimya, moyo wake ulimuuma, alihakikisha kwamba Dylan hajui chochote kile kwa kuwa aliogopa kumpoteza katika maisha yale lakini mwisho wa siku kijana huyo akajua kama yeye hakuwa mama yake, tena katika hali ambayo hata yeye mwenyewe hakuitegemea.

Safari ya kurudi nchini Marekani iliendelea kama kawaida, safari nzima Bwana James alionekana kuwa mwenye furaha tele, alikuwa karibu na Dylan na muda wote alikuwa akimwangalia, moyo wake ulijisikia faraja kubwa.

Mbali na hilo, pia kulikuwa na kitu kilichomtatiza sana kuhusu binti yake, Catherine ambaye alimuahidi kwamba angefanikisha kijana huyo anakuwa mpenzi wake kwa gharama zozote zile.

“Sijui itakuwaje?” alijisema pasipo kujua kama alisikika.

“Kuhusu nini?”

“Catherine, ananiumiza sana kichwa..” alijibu.

“Mwambie ukweli....nadhani kila kitu kimetokea kwa makusudi ya Mungu,” alisema Dylan.

Njiani, Catherine alikuwa askisumbua, kila wakati alikuwa akimpigia simu baba yake, alitaka kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alitaka kufahamu kama mzee huyo alifanikiwa au la.

“Niambie baba...” alisema Catherine.

“Usiwe na presha, tunakuja...” alijibu.

“Umefanikiwa? Niambie ukweli, unaniweka kwenye mshtuko mkubwa...”

“Usijali, nitakuja na utajua kila kitu...” alisema Bwana James.

Walichukua saa ishirini na mbili ndipo wakaanza kuingia nchini Marekani. Kila mmoja alikuwa amechoka. Baada ya kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK jijini New York, wakateremka na kuelekea nje ambapo huko wakakuingia ndani ya magari yao na kuondoka kuelekea nyumbani.

“Dylan...ninamshukuru Mungu hatimaye nimekutana nawe, nilikufikiria kwa kipindi kirefu sana,” alisema Bwana James kwa sauti ya chini huku akionekana kuwa mwenye furaha tele.

Hawakuchukua muda mwingi wakafika nyumbani hapo ambapo gari likaingizwa ndani ya eneo la jumba hilo kubwa. Dylan alibaki akiliangalia jumba hilo tu, hakuamini kile alichokiona, hakuamini kama ingetokea siku ambayo angeweza kuingia katika jumba kubwa kama lilivyokuwa hilo.

Gari lilipoingizwa ndani, wakateremka na kuingia ndani. Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya Bwana James ni kumuita mkewe na mtoto wake, Catherine. Kwa jinsi uso wake ulivyoonekana tu, tabasamu pana wakajua kwamba tayari Dylan alimazana na mzee huyo na hatimaye alikubali kumuoa.

Kitu cha kwanza kabiisa alichokifanya Catherine ni kumsogelea Dylan na kisha kumkumbatia kwa nguvu kama kawaida yake. Tabasamu aliloonyesha baba yake lilimpa uhakika kwamba kila kitu kilikuwa kama kilivyotakiwa kuwa.

“Naomba unioe Dylan, ninaumia jinsi unavyonikataa!” alisema Catherine kwa sauti ndogo, nyororo ya kumtoa nyoka pangoni.

Dylan hakujibu kitu, alibaki akimwangalia msichana huyo. Bwana Dylan alisimama pembeni, alifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Japokuwa alijua kwamba binti yake angeumia sana mara baada ya kumwambia kwamba Dylan alikuwa ndugu yake lakini hakutaka kujali, ilikuwa ni lazima amwambie ili kuepusha mambo mengine.

“Catherine...” aliita Bwana James huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.

“Abeee...”

“Kaa kochini kwanza...” alisema Bwana James huku tabasamu likiendelea kuonekana usoni mwake.

Wote wakakaa kochini. Catherine hakutaka kukaa mbali na Dylan, alikaa pembeni yake huku akiwa na shauku ya kutaka kusikia baba yake angesema nini juu ya kile alichokuwa amemwambia.

“Baba zungumza.....nini kinaendelea?” alijikuta akisema kwa sauti ya chini. Moyo wake ulikuwa na hamu kubwa wa kusikia kile alichotaka kuzungumza baba yake.

Kila mmoja alikuwa na hamu ya kumsikiliza Bwana James alitaka kuzungumza nini kuhusu Dylan. Wote walikuwa na uhakika kwamba mvulana huyo alikubali kuwa naye kwa sababu hata uso wa Bwana James ulionyesha matumaini makubwa baada ya tabasamu kubwa kuonekana usoni mwake.

Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya Bwana James kilikuwa ni utambulisho kwa Bi Leticia ambaye alikuwa pembeni kabisa. Hilo walilifahamu kwamba mwanamke yule waliyekuja naye alikuwa mzazi wa Dylan, wao walichotaka kufahamu ni juu ya Dylan, alikubali kuwa naye, au alikataa.

“Baba, unazunguka sana, tuambie nini kinaendelea,” alisema Catherine huku akionekana kuwa na hamu ya kusikia kile alichotaka kusikia.

“Hakuna ndoa...” alijibu Bwana Dylan kwa kifupi.

“Unasemaje baba?”

“Hakuna ndoa...hakuna tena!” alisema mzee huyo.

Hapohapo Catherine akayahamishia macho yake kwa Dylan, hasira za waziwazi zikaonekana machoni mwake, kile alichozungumza baba yake kilimuumiza moyoni mwake na hakutegemea kusikia kitu kama hicho.

“Kwa nini? Kwa nini unanikataa Dylan, kwa nini hunipendi Dylan?” aliuliza Catherine huku akimkunja shati Dylan ambaye hakuzungumza kitu chochote kile.

Catherine aliumia mno, hakuamini kuona kile alichokisikia kutoka kwa baba yake, japokuwa Bwana James alitaka kufafanua nini kilitokea lakini Catherine akasimama kutoka pale alipokuwa, akatoka nje na kuanza kukimbia mitaani.

Kila mmoja akashtuka, hawakutaka kubaki mahali hapo, walijua jinsi msichana huyo alivyompenda Dylan, kwa kukosa penzi alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile hata kujidhuru.

Wakatoka nje na kuanza kumkimbiza, alikimbia kwa kasi, mtaa mzima ulikuwa kimya na ni yeye tu ndiye aliyekuwa akionekana barabarani. Walikuwa nyuma, walimkimbiza huku wakimuita lakini msichana huyo hakutaka kusimama.

Alipokimbilia ilikuwa ni kwenye jengo kubwa la Motorola lilikokuwa hapohapo New York ambapo halikuwa mbali na mtaa wao ulipokuwa, jengo hilo lilikuwa refu na kulikuwa na floo zaidi ya mia moja.

Japokuwa kulikuwa na walinzi getini na walimuona wakati akija kwa kasi kule walipokuwa, msichana huyo hakusimama, alikimbia, alipofika pale getini akapita kama upepo, alipoingia ndani ya jengo hilo, kitu cha kwanza akaanza kupanda kwenda juu kwa kutumia ngazi.

“Anakwenda wapi?” aliuliza Bwana James huku akionekana kuwa na wasiwasi.

“Anakwenda kujirusha ghorofani,” alijibu Dylan.

Kwa kuwa alikuwa mtu wa mazoezi, akaongeza kasi zaidi, akaingia ndani ya jengo lile na kuanza kupandisha juu huku akimuita Catherine. Alikuwa makini, kila floo aliyofika, alikuwa akiangalia kama msichana yule alikuwa mahali hapo.

Aliendelea kupandisha juu zaidi, alipofika katika floo ya ishirini, akamuona Catherine akiwa amesimama pembezoni mwa ukuta huku akijiandaa kujirusha.

“Catherine...usijirushe, tafadhari usijirushe...” alisema Dylan huku akihema kwa nguvu.

“Utanioa?” aliuliza Catherine huku akiwa anajiandaa kuruka.

“Catherine....”

“Niambie utanioa?” aliendelea kuuliza.

“Catherine, wewe ni ndugu yangu, nitakuoa vipi? Tangu lini mtu akamuoa dada yake?” aliuliza Dylan huku akimwangalia Dylan usoni.

“Nani ndugu yako?”

“Wewe...wewe ni ndugu yangu wa damu, baba yako ni baba yangu pia, zamani alizaa na mwanamke aitwaye Catherine, alipotezana naye kwenye balaa la tsunami, jina lake ndiyo akakupa wewe kama kumbukumbu...Catherine, tunachangia baba, siwezi kukuoa...” alisema Dylan huku akimsogelea Catherine pale alipokuwa.

Catherine hakuamini kile alichokisikia, moyo wake ukapigwa ganzi na akabaki akimwangalia Dylan tu, moyo wake ulichanganyikiwa, alipomwangalia kijana huyo alionekana kufanana kabisa na baba yake, hakuwa na wasiwasi kwamba yule alikuwa ndugu yake.

“Wewe ni ndugu yangu?” aliuliza Catherine, hakuonekana kuamini hata kidogo.

“Ndiyo! Catherine, sikuwa nikilifahamu hili, baba hakuwa akilifahamu pia, yule mwanamke ambaye kila siku nilijua kwamba ni mama yangu ndiye aliyesema ukweli, niliokotwa baada ya mama kufa, akanilea mpaka muda huu,” alisema Dylan, tayari alimfikia Catherine, alichokifanya ni kumvuta na kumkumbatia.

Sauti kubwa ya kilio cha Catherine ikaanza kusikika mahali hapo, aliumia kile alichokisikia, moyo wake ulikosa furaha. Akajuta kuuruhusu moyo wake kumpenda mwanaume ambaye ukweli wa mambo ulieleza kwamba alikuwa ndugu yake wa damu.

Mpaka dakika kumi baadaye, Bwana James na mkewe walifika katika floo hiyo, kila mmoja alionekana kuchoka mno. Hawakuwa peke yao bali walikuwa na watu wengine ambao wote hao walibaki wakiwaangalia kwa mshangao, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

“Watoto wangu...” alisema Bwana James, akawasogelea na kuwakumbatia wote.


Mpaka dakika kumi baadaye, Bwana James na mkewe walifika katika floo hiyo, kila mmoja alionekana kuchoka mno. Hawakuwa peke yao bali walikuwa na watu wengine ambao wote hao walibaki wakiwaangalia kwa mshangao, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

“Watoto wangu...” alisema Bwana James, akawasogelea na kuwakumbatia wote.

****

Dylan alikuwa na ndoto kubwa za kuwa mchezaji mkubwa wa mpira wa kikapu, ila ndoto zake zote zikafa kwa sababu baba yake alitaka asimamie biashara zake kwani kwa jinsi zilivyokuwa, kama angemuachia Catherine, asingeweza kabisa.

Hilo kwake wala halikuwa tatizo, akaanza kusimamia biashara hizo kama alivyoambiwa. Dylan yule kijana aliyekulia kwenye umasikini mkubwa, leo hii hakuwa masikini, alikuwa tajiri aliyekuwa akiogelea katika dimbwi la fedha za baba yake.

Hakuwa mtu wa starehe, hakuwa mtu wa kupenda wanawake kutokana na hali yake kiafya ilivyokuwa. Siku zikaendelea kukatika kama kawaida huku utajiri huo wa baba yake ukizidi kuongezeka kwani usimamizi aliokuwa akiufanya ulikuwa mkubwa na uliojaa umakini.

Kutokana na kuwa kijana mdogo, wanawake wengi walimpapatikia, kila alipopita alionekana kuwa kawaida, hakuwa mtu wa kujikweza, sifa, hayo yalikuwa mambo yaliyomfanya kupata marafiki wengi kila siku.

“Habari yako....” ilisikika sauti ya msichana mmoja, alikuwa ameingia kwenye lifti kupanda juu katika jengo la Kampuni ya Ericom aliyokuwa akimili baba yake nchini Marekani.

Dylan akageuka nyuma kwani mara alipoingia ndani ya lifti hiyo, hakuwa amemuona msichana huyo kutokana na macho yake kuwa kwenye karatasi alizokuwa amezishika. Ndani ya lifti walikuwa wawili tu.

“Salama tu, habari yako binti?” alimsalimia.

“Salama kabisa. Umependeza...” alisema msichana huyo.

“Asante sana.”

Dylan hakutaka kuzungumza neno jingine lolote, alibaki kimya huku macho yake akiyarudisha katika karatasi ile. Alionekana kuwa makini sana na hakutaka kusubiri mpaka afike ofisini kwake kwani kila siku aliokuwa mtu wa kuwa bize tu.

“Naitwa Katty....” alisema msichana huyo huku tabasamu likiwa usoni mwake.

“Nashukuru kukufahamu...”

“Nashukuru pia Dylan...”

Lifti ilipofika katika ghorofa ya saba, Dylan akateremka na kumuacha msichana yule ndani ya lifti ile huku watu wengine wakiwa wamekwishaingia. Akaondoka na kwenda ofisini kwake, kitu cha kwanza kabisa akahitaji ripoti kamili juu ya viporo vyote alivyoviacha jana yake, hivyo akaletewa.

Aliendelea kukaa ofisini, hakuwa mtu wa kutoka, aliwaamini wafanyakazi wake kwamba walikuwa watendaji na hawakuwa watu wa kumuangusha. Walifanya kazi vizuri na kwa kujitoa sana.

Wakati amemaliza kazi zake majira ya saa nane mchana, akachukua begi lake lililokuwa na laptop, akaliweka begani kwa ajili ya kutoka huku akiwa amekwishampigia simu dereva kwa ajili ya kuligeuza gari lake. Wakati anaingiza mkono mfukoni mwake, akahisi kuna kitu, alipoangalia vizuri, mkono wake ukakutana na kikaratasi, akakitoa na kuanza kukiangalia, kwani kumbukumbu zake zilimwambia kwamba kwa siku hiyo hakuwahi hata kukiingiza kikaratasi chochote mfukoni mwake.

‘Maybe, I am in love, see you soon, it’s me, Katty Perrishian...’ (Labda, nipo kwenye penzi zito, nitakuona hivi karibuni, ni mimi, Katty Perrishian...) yalisomeka maneno yaliyokuwa kwenye kikaratasi kile.

Moyo wa Dylan ukapiga paa! Akahisi kwamba aliingiziwa kikaratasi kile na yule msichana wakati wapo ndani ya ile lifti. Akashusha pumzi nzito.

****

Dylan hakumfahamu msichana huyo, hakujua alikuwa nani na alihitaji nini kutoka kwake. Moyo wake ukawa na presha kubwa, hakumkumbuka hata sura yake kwani walipokutana kwenye lifti hakuonekana kujali sana kuhusu yeye, alikuwa na mambo yake hivyo ilikuwa vigumu mno kuikumbuka sura yake.

Hakutaka kujali sana, akarudi nyumbani kwake na kutulia. Alikuwa kwenye hali ya kawaida tu, akafungulia televisheni na kuanza kuangalia mchezo wa kikapu uliokuwa ukiendelea kati ya Chicago Bulls na La Lakers. Hakutaka kumtilia maanani msichana huyo, aliamua kwa moyo mmoja kufanya mambo yake kwani alikumbuka vizuri kwamba hakuwa salama kiafya na hilo tatizo hakutaka lijulikane na mtu yeyote yule.

Ulipofika muda wa kulala, akajikuta akianza kukikumbuka kile kikaratasi kilichoandikwa ule ujumbe aliopewa. Ulikuwa ujumbe mfupi lakini wenye kusisimua sana. Kwa kipindi hicho, hakutaka kuwa na msichana yeyote yule, mawazo yake yalikuwa kwenye kazi tu. Alipoona ameshindwa kabisa kujikontroo, akachukua simu yake na kumtumia ujumbe wa maneno mdogo wake, Catherine.

“Kama utakuwa na nafasi kesho, naomba nikuone,” aliandika uumbe huo kwenye simu yake na kumtumia Catherine.

“Kuna nini?”

“Hakuna kitu cha kutisha, naomba nikuone kwanza...’

“Sawa...”

Usingizi haukumpata, alikuwa kwenye mawazo tele, alijaribu kuuvuta kwa kbimbilika huku na kule lakini hakulala mpaka ilipofika majira ya saa sita usiku ndipo akalala usingizi mzito.

Asubuhi alipoamka, kitu cha kwanza kilichokuja kichwani mwake kilikuwa ni juu ya yule msichana, bado alikisumbua kichwa chake japo kuukumbuka uso wake lakini hilo halikuwezekana.

Akaelekea bafuni, akaoga na kisha kujiandaa kwa ajili ya kuonana na Catherine kabla ya kwenda ofisini kwake. Jambo kama hilo, hasa kuhusu msichana hakutaka liwe peke yake, alimzoea Catherine, alikuwa ndugu yake na rafiki yake wa karibu ambaye mara kwa mara alikuwa naye na kushauriana mambo mbalimbali kuhusu maisha.

“Huyo msichana ni nani?” aliuliza Catherine.

“Simfahamu kabisa...”

“Na haujawahi kumuona kabla?”

“Ndiyo! Na hata pale nipomuona, sikumtilia maanani..” alijibu Dylan.

Catherine ndiye alikuwa mshauri wake lakini mpaka muda huo hakujua ni kwa namna gani alitakiwa kumshauri Dylan ambaye alionekana kutamani sana kuambiwa neno lolote lile kuhusu msichana huyo.

Hiyo ilikuwa siku ya pili, alitegemea kumuona msichana huyo siku hiyo lakini palikuwa patupu. Katika hali ya kushangaza kabisa, mawazo yakaanza kumsumba, hakuwa na furaha, muda wote alikuwa kimya ndani ya ofisi yake akimfikiria msichana huyo.

Ukimya huo haukuishia siku hiyo tu, ilikatika wiki ya kwanza, msichana huyo hakutokea, wiki ya pili ikakatika lakini bado msichana huyo hakuweza kutokea kitu kilichompa maswali mengi kwani naye kwa kipindi hicho alitamani sana kumuona msichana huyo.

Wiki ya tatu ilipoingia huku mawazo juu ya msichana huyo yakiwa yamepungua kichwani mwake ndipo sekretari wake alipompigia simu na kumwambia kwamba kulikuwa na mzigo wake na ulikuwa umeletwa na msichana fulani ambaye hakujitambulisha.

“Mzigo wa nini?” aliuliza kwenye simu.

“Maua...”

“Maua?”

“Ndiyo bosi! Nikuletee?” aliuliza sekratari.

“Niletee...”

Ndani ya sekunde kadhaa, msichana huyo akaufungua mlango na kuingia ndani, moja kwa moja akaenda katika meza aliyokuwepo bosi wake kisha kumpa maua yale.

Ndani ya sekunde kadhaa, msichana huyo akaufungua mlango na kuingia ndani, moja kwa moja akaenda katika meza aliyokuwepo bosi wake kisha kumpa maua yale.

Dylan akayachukua, kitu cha kwanza kabisa ilikuwa ni kuyanusa, yalinukia vizuri, harufu yake ilimvutia mno. Yalikuwa maua ya kila rangi, yaliyopendeza machoni mwake.

“Nashukuru,” alimwambia mfanyakazi wake na kutoka.

Alibaki akiyaangalia, kila wakati moyo wake ulihisi kitu fulani hivi ambacho wala hakupata wakati mgumu kutambua kilikuwa kitu gani, yalikuwa ni mapenzi ya dhati.

Hakutaka kabisa kitu hicho kitokee, aliufahamu moyo wake, aliifahamu afya yake ambayo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya kuwakataa wanawake waliokuwa wakimfuatilia, kitu ambacho kilimpa maswali ni juu ya huyu msichana ambaye wala hakumkumbuka sura, alikuwa amempenda tu kutokana na vitu alivyokuwa amemfanyia.

Maua yale yalikuja kama yalivyokuja, hakukuwa na kitu kingine kama watu wengine wanavyofanya kwamba kuna jina, namba ya simu na hata mahali yalipotoka.

Siku hiyo kazi hazikufanyika, kila wakati macho yake yalikuwa kwenye maua yale ambapo muda wa kutoka ulipofika, akayachukua, akayaingiza ndani ya gari na kisha kuondoka zake kuelekea nyumbani.

Huo ndiyo ukawa mwanzo, hakuishia kupokea maua, aliendelea kupokea zawadi mbalimbali za kimapenzi ambazo zilimchanganya. Alipagawa, hakujua Katty alikuwa wapi na alihofia nini kurudi tena katika jengo lile kwa ajili ya kumuoa.

Katika siku ambayo aliletewa boksi lililokuwa na nguo za kiume ndiyo siku ambayo alichanganyikiwa zaidi baada ya kuona anuani iliyomuenyesha kwamba mzigo huo ulitumwa kutoka nje ya nchi, tena Ulaya nchini Ufaransa.

“Duh! Hayupo Marekani tena?” alijiuliza.

Ndani ya boksi hilo kulikuwa na cd ambayo aliichukua na kuiweka kwenye kompyuta yake na kuanza kuitazama. Picha alizozikuta humo zikamfariji, akamuona msichana mwenyewe, alikuwa msichana mrembo mno na kila picha iliyokuwa ikionekana ilibeba ujumbe mzito ulioandikwa kwa lugha mbili, yaani Kiingereza na Kiitaliano.

“Te amo,” (Nakupenda) lilikuwa neno pekee la Kiitaliano ambalo alilielewa.

Uso wake ukawa kwenye tabasamu pana, moyo wake ukajisikia faraja kubwa, mapenzi yakaongezeka zaidi, kiu ya kumuona msichana huyo ikamshika zaidi.

Huo ulikuwa mwezi wa kwanza, hakukuwa na kitu alichokuwa akikitamani kama kuonana na msichana huyo. Mwezi wa pili ulipoingia, akatumiwa zawadi ya gari ambayo ilipelekwa mpaka ofisini kwake.

Japokuwa alikuwa bilionea lakini zawadi ile ya gari ambayo alipelekewa ilikuwa bab’ kubwa kwake. Hakuamini kama msichana huyo angeweza kumletea gari ya thamani kama hilo.

Akatokea kulipenda kutokana na jinsi lilivyokuwa ila pamoja na hayo yote, akalipenda zaidi kwa kuwa lilikuwa ni zawadi kutoka kwa msichana aliyehisi kwamba alikuwa na mapenzi mazito juu yake.

Pale lilipoegeshwa, kila mtu alikuwa akilishangaa, lilikuwa zuri, aina ya Porsche lenye gharama kubwa na lilikuwa la kisasa zaidi. Wengi wakahisi kwamba bosi wao Dylan ndiye alikuwa amelinunua, wengi wakampongeza pasipo kujua kwamba lile lililetwa kama zawadi kutoka kwa msichana ambaye hakuwahi kumuona uso kwa uso zaidi ya mara moja.

Miezi ikakatika, mwaka wa kwanza ukapita, bado aliendelea kupokea zawadi tu, kulikuwa na jina, ila hakukuwa na anuani yoyote, akabaki akiwa amechanganyikiwa tu. Alitamani hata kuisikia sauti yake.


Siku ziliendelea kukatika, bado moyo wake ulikuwa na shauku kubwa ya kumuona msichana huyo, akutane naye na kuzungumza naye kwani kuna mengi alitaka kumwambia hasa jinsi alivyokuwa akijisikia kwa kipindi hicho.

Siku hazikumsubiri, ziliendelea kukatika kama kawaida na kila wiki ilikuwa ni lazima kupokea zawadi yoyote kutoka kwa msichana huyo ambaye bila hofu yoyote ile alikuwa amempenda kwa mapenzi ya dhati.

Baada ya mwaka huo kukatika, mwezi wa sita ndipo akapokea simu. Kwanza alipokiangalia kioo, ilionyesha kwamba haikuwa simu kutoka nchini Marekani, ilitoka nje kabisa hasa kwenye nchi za Ulaya.

Kwanza hakufikiri kama mpigaji alikuwa Katty, alichojua ni kwamba mpigaji wa simu hiyo alikuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa ambao alikuwa akifanya nao biashara, alichoamua ni kuipokea.

“Habari...” ilisikika sauti nzuri ya msichana.

“Salama...”

“Bila shaka naongeza na Dylan....”

“Ndiyo! Wewe nani tafadhali?”

“Naitwa Katty, sijui unanifahamu?”

Aliposikia jina hilo tu, moyo wake ukapiga paa, hakuamini kama baada ya kusubiri kwa muda wa mwaka mmoja na nusu hatimaye msichana huyo alimpigia simu na kuzungumza naye.

Alichokifanya ni kuangalia tena kioo cha simu yake, furaha aliyokuwa nayo kipindi hicho haikuweza kuelezeka hata mara moja.

“Mbona unanitesa namna hii?” aliuliza Dylan.

“Nakutesa? Kivipi?” aliuliza msichana huyo.

“Kwa nini unanitumia zawadi?”

“Kwa sababu nakupenda!”

“Sasa huoni kama zawadi hizo zinaweza kubadilisha moyo wangu na mimi kukupenda?” aliuliza Dylan kwa sauti ya chini.

“Kwa hiyo nimefanikiwa?”

“Kufanikiwa nini?”

“Kuuteka moyo wako?”

“Tena sana tu...”

Walikuwa wakizungumza kwenye simu huku kila mmoja akionekana kumpenda mwenzake, walizungumza mengi na hata simu ilipokatwa, bado waliendelea kuwasiliana kila siku.

Msichana Katty hakuwa mtu wa kutulia, alikuwa ni wa kwenda huku na kule. Kama ilivyokuwa kwa Dylan kuwa mtoto wa bilionea, hata Katty naye alikuwa hivyohivyo huku baba yake ndiye akiwa mwanzilishi wa kampuni ya magari ya Ferrari.

Kitu alichokitamani Dylan ni kumuona tena msichana huyo ana kwa ana, japokuwa alikuwa akitumiwa video za msichana huyo lakini hilo wala hakuridhika nalo hata kidogo, kitu alichokitaka ni kumuona tu.

Siku zikaendelea kukatika, kila wiki ilikuwa ni Katty kusema kwamba angerudi siku fulani, siku hiyo ilipokuwa ikifika, ilikuwa kimya hivyo kupanga siku nyingine.

Dylan alichanganyikiwa, kama kupenda, muda huo moyo wake ulikuwa kwenye hatua za mwisho kabisa. Hakutaka kusikia la mtu yeyote yule, alichokuwa akikitaka ni Katty tu.

Baada ya mwaka wa pili kuingia, akajikuta akianza kuingia kwenye urafiki wa karibu na binti mwingine ambaye alikuwa akifika sana ofisini kwake kwa ajili ya kuweka mpangilio mzuri wa ofisi (office designing), binti huyo mrembo aliitwa Pauline Mendez.

Msichana huyu alikuwa mrembo hasa, baba yake alikuwa masikini aliyekuwa na asili ya Mexico huku mama yake akiwa Mmarekani mweusi. Alikulia katika maisha ya kimasikini na mama yake aliyekuwa akisumbuliwa na kansa ya titi.

Alipambana sana katika maisha yake, alitafuta fedha kwa ajili ya kumtibu mama yake. Siku zote alikuwa mtu mwenye huzuni kubwa, alitafuta sana kazi, alipopata, nusu ya mshahara wake ulikwenda kwa mama yake.

Baba yake ambaye alikuwa akiishi nchini Mexico naye alikuwa masikini wa kutupwa, alifilisika baada ya kuendekeza sana mchezo wa kamari. Kwa sababu alikuwa na utaalamu wa kutengeneza ofisi ziwe na muonekano mzuri, akaajiliwa na kampuni moja.

Kila siku ilikuwa ni lazima kufika katika jengo la kampuni hiyo aliyokuwa akiisimamia Dylan. Kila mtu aliyemuona Pauline, alimpenda kwani sura yake ya kipole ilimpagawisha kila mtu.

Jinsi ya kumuingia Pauline ilikuwa kazi ngumu, muda mwingi alionekana kuwa bize na mambo yake, hakuwa mtu wa kujichanganya na kila alipoingia katika ofisi hiyo, alikuwa mkimya, haongei mpaka alipoongeleshwa.

“Yule dada amefika bosi...” alisema sekratari wa Dylan kwenye simu.

“Yupi?”

“Yule wa kupamba ofisi...”

“Mwambie aingie...”

Dylan alikuwa bize na mambo yake, japokuwa kila siku msichana huyo alikuwa akifika hapo lakini hakuwa amepata muda wa kumuona zaidi ya kuona ofisi zikipendeza lakini mpendezeshaji hakumfahamu.

Baada ya sekunde kadhaa, msichana Pauline akaingia ndani ya ofisi yake, akamkaribisha, akakifuata kiti na kutulia. Alimwangalia, sura yake tu ilionyesha ni jinsi gani alikuwa mpole, ila kwa sababu kichwa chake kilikuwa na uwezo mkubwa, akagundua kwamba msichana huyo hakuwa sawa, alikuwa na maumivu makubwa moyoni mwake.

“Unaitwa nani?”

“Pauline Mendez...”

“Samahani! Wewe ndiye mbunifu wa ofisi zetu?” aliuliza Dylan.

“Ndiyo!”

“Hongera sana, unajitahidi sana kufanya kazi, ila naruhusiwa kukuuliza swali?” aliuliza Dylan.

“Niulize tu...”

“Kuna nini kinakusumbua moyoni mwako?”

“Hakuna kitu..”

“Hapana Pauline, haupo sawa, unaonekana kama mtu aliyekata tamaa, aliyepoteza matumaini, mwenye huzuni kubwa, tatizo ni nini?” aliuliza Dylan huku akimwangalia msichana huyo usoni.

Pauline hakujibu kitu, alinyamaza, akakiinamisha kichwa chake chini, alipokiinua, machozi yalikuwa yakimtoka. Alichokisema Dylan kilikuwa kweli kabisa, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali kwa sababu ya mama yake aliyekuwa mgonjwa.

Hakujua kama ilikuwa sahihi kumwambia Dylan au la. Alichokifanya Dylan ni kusimama na kuanza kumfuata msichana huyo. Alipomfikia, akaupeleka mkono wake begani kwa msichana huyo, akamuinamia, akakitoa kitambaa chake, akaanza kumfuta machozi.

*****

Machozi hayakutoka hivihivi, kitu alichohisi Dylan ni kwamba kulikuwa na kitu kikubwa sana kilichokuwa kikimsumbua msichana Pauline na ndiyo maana akaamua kumsogelea na kumfuta machozi yake.

“Kuna nini?” aliuliza Dylan kwa sauti ya chini.

“Inaniuma...”

“Nini tatizo?”

Pauline hakujibu swali hilo, alibaki kimya huku akiugumia kwa kwikwi mfululizo. Moyoni mwake, picha ya mama yake akiwa kitandani ikamjia, alikuwa kwenye mateso makubwa, alikosa msaada kwa kuwa hakuwa na fedha za kutosha.

“Mama yangu ni mgonjwa,” alisema msichana huyo.

“Anaumwa nini?

Hapo ndipo Pauline alipoanza kumuhadithia Dylan kile kilichokuwa kikiendelea kwa mama yake. Historia yake ilimuumiza mno Dylan na kitu pekee kilichomgusa kuliko vyote ni jinsi alivyokuwa akitumia zaidi ya nusu ya mshahara wake kwa ajili ya mama yake.

Huruma nyingi ikazidi kumuingia Dylan, maumivu aliyokuwa nayo msichana yule aliamini kwamba angeweza kuyaondoa kwani hata kiasi ambacho kilihitajika hospitalini, kwake kilikuwa kidogo mno.

Alichomwambia ni kwamba angemfanyia mambo yote likiwemo hilo la kumtibu mama yake mpaka kuhakikisha anapona au kama si kupona basi kuwa na nafuu. Kwa Pauline maneno hayo kwake yalikuwa kama ndoto, hakuwahi kuamini kama kuna siku kungetokea mtu ambaye angekuwa tayari kumsaidia mama yake kwa ule ugonjwa aliokuwa akiugua na kumlaza kitandani.

Siku hiyo, alichokifanya Dylan ni kumchukua Pauline na kuondoka naye kuelekea huko nyumbani. Kwa kumwangalia, alikuwa msichana mrembo, aliyevutia mno lakini nyumba aliyokuwa akiishi na mama yake haikuendana na urembo wake kabisa.

Wakaingia ndani, moja kwa moja Dylan akapelekwa katika chumba alicholazwa mwanamke huyo. Chumba kilikuwa ni cha hadhi ya chini na mwanamke huyo alikuwa kwenye hali mbaya mno.

Dylan akashindwa kujizuia, hapohapo machozi ya uchungu yakaanza kububujika mashavuni mwake, hali aliyoikuta kwa mwanamke huyo hakika ilimuumiza mno. Akapiga hatua kumsogelea, alipomfikia, akamshika mkono.

“Pole sana mama...” alijikuta akimwambia.

“Asante sana...koh...koh...koh...” aliitikia na kukohoa.

Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumsaidia katika matibabu, kitu cha kwanza kabisa alichokifanya kwao ni kuwatafutia nyumba nyingine ambayo ilipatikana siku hiyohiyo, tena ilikuwa na kila kitu ndani.

Hakuishia hapo tu bali alimpeleka mwanamke yule katika hospitali kubwa ya Herieth Medical Center hapo New York kwa ajili kufanyiwa matibabu ambayo yangegharimu dola elfu hamsini ambazo ni zaidi ya shilingi milioni mia moja.

Fedha kwake halikuwa tatizo lolote, kitu alichokuwa akikitamani wakati huo ni kumuona mwanamke huyo akipona na kuwa mzima kabisa. Siku zikaendelea kukatika, hakuacha kumtembelea hapo hospitalini.

Kwa Pauline, kila kitu kilichoendelea kwake kilionekana kuwa kama ndoto, hakuamini kama katika dunia hii kungekuwa na mtu aliyekuwa na roho nzuri kama alivyokuwa Dylan.

Kupitia msaada huo, akajikuta akianza kumpenda kijana huyo, mara kwa mara alikuwa akimfikiria kichwani mwake. Moyo wake ukawa na hamu ya kuwa naye, kila alipojilaza kitandani, hakumfikiria mtu yeyote zaidi ya Dylan tu.

Kile alichofanyiwa, akatamani kukilipa kwa kulala naye tu na ikiwezekana kumpa mapenzi yake yote. Hakuwa na fedha hivyo malipo ambayo kwake aliyaona kufaa ni kumpa penzi zito ambalo asingeweza kusahau katika maisha yake yote.

Hata kabla ya kumwambia kile alichojisikia moyoni mwake akaanza kumfuatilia mwanaume huyo kama alikuwa na mpenzi au la! Kama asingekuwa karibu naye lingekuwa suala gumu sana kumchunguza hivyo alichokifanya ni kuomba kazi katika kampuni ya Dylan kitu ambacho kilikubaliwa haraka sana pasipo kujua lengo la msichana huyo.

Kila siku ilikuwa ni lazima kuonana naye, wanazungumza kisha kuendelea na ishu nyingine. Kwa Dylan, hakuweza kugundua kitu chochote kile, kwake, msichana huyo alionekana kuwa wa kawaida sana hivyo kumchukulia kama rafiki yake jambo ambalo halikukubalika kabisa kichwani mwa msichana huyo.

“Nina shida...” alimwambia Dylan.

“Ipi?”

“Ninataka kutoka mtoko wa usiku na wewe,” alimwambia.

“Na mimi?”

“Ndiyo! Ninaomba...” alimwambia kwa upole mwingi.

“Hapana Pauline, siwezi kufanya hivyo!”

“Kwa nini?”

“Nina mambo mengi sana, labda mwezi ujao...”

“Una uhakika itawezekana bosi?”

“Napo tutaangalia pia...”

Jibu hilo hakulipenda, lilimuumiza moyoni mwake lakini hakuwa na jinsi, alifahamu kwamba Dylan alikuwa tajiri, mtu ambaye hakutaka kabisa kuonekana na watu wengi na ndiyo maana muda mwingi alishinda ofisni kwake ila pamoja na hayo yote, aliona kuna kila sababu ya kutoka mtoko wa usiku na mwanaume huyo.

Hakukuwa na kingine alichokifanya zaidi ya kuwa na subira, kwa sababu aliambiwa kwamba mwezi mmoja, basi akaona litakuwa suala la busara na linalohitaji uvumilivu kama tu angesubiri.

Siku ziliendelea kukatika, hakuacha kumwambia Dylan kuhusu ahadi yao na bado mwanaume huyo alimwambia kwamba wangekwenda tu. Baada ya mwezi kukatika, msichana huyo akamfuata Dylan ofisini kwake na kumuuliza kama alikuwa tayari.

“Tufanye Jumamosi...” alisema, siku hiyo ilikuwa Jumatatu.

Kwa Pauline hakuamini, kwake, alikuwa na furaha mno na muda wote uso wake ulikuwa ni wenye kutabasamu tu. Siku zikakatika na ilipofika Ijumaa, akapata taarifa kwamba usiku wa siku hiyo Dylan alikuwa akipanda ndege kuondoka kuelekea Qatar kwani kuna wafanyabiashara wa mafuta alitaka kuzungumza nao.

Moyo wake uliumia mno, hakuamini kama kweli ilishindikana kwake kuonana na mwanaume huyo na hatimaye amchukue na kutoka naye mtoko wa usiku. Usiku wa siku hiyo alishindwa kulala, alibaki akilia tu kwani kilichotokea kilimuumiza mno.

Mama yake alimshangaa, alimfahamu vilivyo binti yake, kila alipokuwa na furaha, alijua hilo na hata alipokuwa na huzuni, alilijua hilo. Usiku wa siku hiyo alipoingia chumbani kwake, binti yake hakuwa kama alivyokuwa, macho yake yalikuwa mekundu na ilionyesha kwamba alikuwa na huzuni sana tofauti na kipindi kilichopita.

“Kuna nini?” aliuliza mama yake kwa sauti ya chini, tena huku akiwa karibu naye kabisa.

“Inaniuma mama...”

“Inakuuma nini?”

“Dylan mama...”

“Amefanya nini?”

“Ameondoka kwenda Qatar.”

“Sasa ndiyo uumie?” aliuliza mama yake, Pauline hakujibu swali hilo, kilio kikaanza upyaaaa.


“Dylan mama...”

“Amefanya nini?”

“Ameondoka kwenda Qatar.”

“Sasa ndiyo uumie?” aliuliza mama yake, Pauline hakujibu swali hilo, kilio kikaanza upyaaaa.

*****

Mama yake alijitahidi kumbembeleza lakini msichana huyo haikuwa rahisi kunyamaza, moyoni mwake kulikuwa na maumivu makali, mapenzi yaliyokuwa yalikuwa makubwa mno, hakutaka kuona Dylan akifanya kitu chochote kile ambacho hakutaka kukifanya, yaani kama alimwambia ni lazima kwenda mtoko wa usiku, basi watoke.

Mpaka mama yake anaondoka chumbani humo, hakurudi katika hali yake ya kawaida, bado alikuwa na huzuni tele huku muda mwingine akilia kama kawaida yake.

Alijuta kuuruhusu moyo wake kumpenda mtu ambaye wala hakuwa na habari naye, alishindwa kuelewa ni kitu gani kingetokea kama tu angepata taarifa kwamba Dylan alikuwa na mwanamke mwingine.

Alihisi angekufa kama angesikia hivyo, na kama si kufa basi angeweza kuathirika kiafya kwani tayari akili yake ilichanganyikiwa kwa mapenzi mazito aliyokuwa nayo kwa mwanaume huyo.

Hakuacha kuwasiliana naye, hakuacha kuzifikisha hisia zake kwamba mwanaume huyo aliondoka katika siku ambayo alimhitaji sana, hakuacha kumwambia kuhusu huzuni yake, yote hayo, alimwambia wazi ili afahamu.

“Utanisamehe, ilikuwa ni ghafla sana, nilihisi angekwenda baba au Catherine, matokeo yake nimekuja mimi,” alisema Dylan kwenye simu, kwanza kitendo cha kuombwa msamaha tu, kikaonyesha ni jinsi gani alikuwa na thamani kubwa kwa mwanaume huyo.

“Na unarudi lini?” aliuliza Pauline.

“Sijajua, ila ningependa nirudi Jumatatu...”

“Nitafurahi sana kukuona..”


ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako hapa

  Facebook Google+ Twitter LinkedIn Tumblr Menu SKIP TO CONTENT HOME WAKUBWA TU 18+ WAANDISHI WA SIMULIZI SIMULIZI ZA SAUTI UCHAWI UPO SHUHU...